TIMU ya Kijitonyama Veterans yenye maskani yake Kijitonyama,
leo imefanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi wapya wa kuingoza timu hiyo kwa
kipindi cha miaka mitano.
Nafasi
zilizokuwa zikigombewa ni tisa, ambapo katika nafasi ya Mwenyekiti
aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo muda uliopita, Lupyana Michael,
ameendelea kubaki katika nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura na wajumbe
na kuongoza dhidi ya mpinzani wake, Petro Malima .
Pia
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Timu hiyo Amon Petro, naye ameendelea kubaki
katika nafasi hiyo baada ya kuibuka na kura nyingi zaidi ya mpinzani
wake, Evodius Mtawala
Naye
Mratibu wa timu hiyo, Majuto Omary,pia ameendelea kubaki katika nafasi
hiyo baada ya kuibuka kidedea dhidi ya mpinzani wake Evans Malla,
Kwa
mujibu ya utaratibu wa Timu hiyo, kutokana na mapendekezo ya Wajumbe,
katika uchaguzi, majina mawili yanayopigiwa kura na mmoja kati yao
anayepata kura nyingi ndiye anapaswa kuwa kuwa kiongozi katika nafasi
husika na anayefuatia kwa kura anakuwa msaidizi.
VIONGOZI WALIOCHAGULIWA:-
MWENYEKITI: Lupyana Michael
MAKAMU MWENYEKITI: Malima Petro
KATIBU MKUU: Amon Petro
KATIBU MSAIDIZI: Evodius Mtawala
MRATIBU MKUU: Majuto Omary
MTARIBU MSAIDIZI: Evans Malla
MWEKAHAZINA MKUU: Othaman Hussein
MWEKA HAZINA MSAIDIZI: Sweetbert Mwombeki
MSEMAJI WA TIMU: Muhidin Sufiani (Mafoto)

Baadhi ya wajumbe wakipitia vifungu vya katiba wakati wa uchaguzi huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...