Kampuni ya Magazeti ya Serikali Tanzania Standard Newspapers (TSN) wachapaji wa magazeti ya Daily News, Sunday News, Habarileo, Habarileo Jumapili na Spotileo imeadhimisha miaka 10 tangu kuanza kwa gazeti la Habarileo mnamo Desemba 21, 2006 kwa kukata keki huku Uongozi wa Kampuni hiyo ukitangaza shamra shamra za mwezi mmoja wa kusherehekea kuzaliwa kwa gazeti hilo.
Aidha ili kushirikiana na wadau wengine, Kampuni imetangaza punguzo la asilimia 30 kwa mteja atakeatangaza tangazo lake ndani ya siku 30 za shamrashamra katika gazeti la Habarileo.
Miongoni mwa wageni maalum waliohudhuria sherehe hizo ni Mhariri Mtendaji wa zamani wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Isack Mruma (wapili kulia) ambaye kwa sasa ni Ofisa wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambaye alishiriki kukata keki pamoja na Mhariri Mtendaji wa sasa Dk Jim Yonaz (wapili kushoto) na Naibu Mharidi Mtendaji, Tuma Abdallah. Kushoto akishuhudia ni Meneja Mauzo na Masoko, Januarius Maganga.
Isack Mruma akizungumza katika shamra shamra hizo na kuelezea changamoto mbalimbali alizokumbana nazo tangu kuanza kwa gazeti hilo.
Wafanyakazi wa TSN wakifuatailia
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...