Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MSTAHIKI meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe amesema kuwa eneo litalakolokuwa limepimwa na kugundulika ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii kama Manispaa wapo tayari kulipa fidia kwa wananchi ili kupisha.

Hayo ameyasema leo kwenye mkutano na wananchi wa mtaa wa Kunguru, kata ya Goba wakiwa pamoja na taasisi binafsi inayijishughulisha na masuala ya upangaji na upimaji wa maeneo nchini HUSEA. 

Jacob amesema, anatoa sifa kubwa sana kwa hatua iliyofikiwa na wananchi wa Kunguru kwa kuamua kupima maeneo yao wenyewe na zaidi kwani Halmashauri ndiyo wenye majukumu ya kufanya hivyo ila kwa hatua hiyo waliyofikia kwa kushirikiana na HUSEA wamefanya jambo kubwa sana na wanawaunga mkono kwa jitihada hizo. 

"Kutakapotokea kama kuna eneo ambalo ni eneo la wazi au kwa ajili ya huduma za kijamii na limejengwa na mkakubaliana kupata eneo lingine kwa ajili ya shughuli hizo basi msisite kutuambia kwani ili sisi kama Halmashauri tuweze kulipa fidia, "amesema Jacob. 

Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa amesema kuwa kwa hatua hii imeweza kusaidia katika kupanga maeneo ya mtaa wa Kunguru na zaidi wananchi wameweza kushirikiana nao kwa hatua nzuri mpaka kufikia kuweka makubaliano ya upangaji wa maeneo na kuna baadhi ya wananchi wamejitolea kuacha maeneo yao kwa ajili ya kuendeleza mipango endelevu. 

Katika eneo la Kunguru, kumeweza kupatikana kwa maeneo 1432 na wameweza kuyapima na waliweza kupata ushirukiano mzuri kutoka kwa Wizara ya Ardhi na waliweza kuwapa ramani halisi ya eneo hilo ila kutokana na wanachi tayari wameshajenga wamepata sura ya ramani ambayo ni mpya na itakapokamilikwa kupimwa kuanzia mwezi Januari mwakani watafanya mabadiliko ya ramani hiyo. 

Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala amesema kuwa wao kama Wizara wamedhamiria kuhakikisha wanashirikiana na makampuni binafsi kuweza kupima na kupanga maeneo ya makazi ya watu mjini na vijijini na zaidi mpaka kufikia mwaka 2016 ni asilimia 15 tu ya maeneo yamepimwa. 

Mradi huo ulianza mnamo mwezi Mei mwaka huu na uliweza kupata changamoto mbalimbali kutoka kwa wananchi ikiwemo watu kusema kuwa ni makampuni ya kitapeli ila baada ya kuwapa elimu waliwez kuelewa na siku ya kwanza ya mkutano huo wananchi zaidi ya 800 walijiandikisha kwa ajili ya kupimiwa maeneo yao. 
Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jacob Masawe akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji na Upimaji wa eneo hilo unaoendeshwa na Kampuni ya HUSEA, kulia ni Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa na kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala 
Mwenyekiti wa HUSEA, Renny Chiwa .

akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kunguer kata ya Goba wakati wa Mkutano wa Upangaji na Upimaji wa eneo hilo na kuelezea namna kampuni yake ilivyojikita katika kuhakikisha wanasaidiana na serikali kwenye utatuzi wa migogoro na upangaji wa maeneo. Akiwa amekaa meza moja na Diwani wa kata ya Goba Ibrahim Kenya (wa kwamza kushoto), Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji, Prof John Lupala. 
Wananchi wakiwa wanaelezewa namna Mtaa wa Kunguru ulivyopimwa na kutakiwa kupangwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...