Na: Frank Shija –MAELEZO

WAKAZI wa Pangani waaswa kujitokeza kwa wingi katika wiki moja ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara inatarajia kuanza siku ya Desemba 7 mwaka huu.

Wiki hiyo inalenga kutoa fursa kwa wananchi kuelezea ,kusikilizwa na kutatuliwa kero zao zinazohusu masuala mbalimbali ikiwemo rushwa na ufisadi.Kauli hiyo imetolewa jana (leo) na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi.Zainab Abdallah alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi katika mahojiano maalum kuhusu maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara. 

Bi. Zainabu amesema kuwa katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru Wilaya yake imeandaa Wiki ya Uhuru ambayo itatumika kwa Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mahakama na Serikali kwa ujumla kusikiliza kero za wananchi hasa zinazohusu masuala ya Rushwa na Ufisadi.

“Mimi kama mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Mahakama nimemzungumza na Mahakimu kujitahidi kuharakisha usikilizwaji wa kesi zote zinazohusiana na rushwa kwani mueleke wa Serikali yetu ni kutokomeza rushwa kabisa,” alisema Bi. Zainab.Aliongeza kuwa Wilaya yake imeamua kuandaa wiki hii ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamo ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kukabiliana na adui rushwa na ufisadi kwa vitendo.

Amesema kuwa kutokana na dhamira ya dhati aliyonayo Mhe. Rais Magufuli katika kukabiliana na rushwa na ufisadi ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkoni jitihada hizo.

“Ni wahakikishie Watanzania kwamba Serikali yao imedhamiria kwa dhati kubwa kuhakikisha inatokomeza tatizo la rushwa na ufisadi kwani watu wamekuwa wakihujumu uchumi wa taifa katua Awamu hii haitafumbia macho watu wa namna hiyo,” alisisitiza Bi. Zainabu.

Aidha ameongeza kuwa mbali na kusikiliza kero za wananchi wiki hiyo pia itatumika kuhamasisha wajasiriamari wadogo wadogo kuanzisha viwanda ili kutekeleza azma ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.Desemba 9 kila mwaka Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kwa mwaka huu kitaifa yatafanyika Dar es salaam na kauli ya mwaka huu ni “Tuunge Mkono Jitihada za Kupinga Rushwa na Ufisadi na Kuhimarisha Uchumi wa Viwanda kwa Maendeleo ya Nchi Yetu.”

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...