Na. Ahmad Mmow, Nachingwea.

Waendesha pikipiki za kusafirisha abiria (bodaboda) wilayani Nachingwea wameaswa wasikubali kutumiwa na wanasiasa nakufanywa ngazi ya kufikia malengo yao yakisiasa.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na mkurugenzi mtendaji wa taasisi isiyo ya kiserikali ya kupambana na umasikini na utunzaji mazingira (APEC), Respicius Timanywa.Wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya usalama barabarani iliyofanyika katika kijiji cha Chiola wilaya ya Nachingwea.

Timanywa alisema madereva bodaboda ni kundi lenye nguvu katika jamii kutokana na kuundwa na vijana. Hivyo baadhi ya wanasiasa wamekuwa natabia ya kuwalaghai ili wawaunge mkono kwa kuwataka washiriki kutekeleza vitendo vya uvunjifu wa sheria. Ikiwamo kushiriki maandamano na mikutano isiyo halali.

Mkurugenzi huyo ambae taasisi yake inashugulika pia na kupunguza maafa kwa waendesha pikipiki, alisema vijana hawana budi kukataa kutumika kufanya vitendo vitakavyo vuruga amani na utulivu uliopo nchini kwa maslahi ya wanasiasa.

Badala yake wajiwekee malengo ya kufikia maendeleo kwakufanya kazi kwa juhudi na maarifa."Anzisheni vikundi vya ujasiriamali na fungueni akaunti ili muweze kuungwa mkono na serikali, muweze kukopeshwa kupitia fedha za mifuko ya vijana na wanawake," alisisitiza Timanywa.
Waendesha Boda Boda wakisubir abiria

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...