Kamati
ya kuwezesha na kuboresha usafiri wa anga ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imekutana kwa siku tatu mjini
Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mikakati ya
nchi wanachama kuboresha sekta hii ya uchukuzi katika nchi wanachama.
Mkutano
huo wa 41 umefunguliwa rasmi na Waziri
wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Balozi Ali Abeid Amani Karume, ambaye amesema
miundombinu katika viwanja vingi vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki vinahitaji kuboreshwa ili kumudu
ushindani wa kibiashara katika sekta hii.
Aidha, amezungumzia umuhimu wa nchi wanachama
kupunguza tozo kwa kampuni zinazotoa huduma za usafiri wa anga ili kuvutia
uwekezaji zaidi katika sekta.
Waziri
huyo amesisitiza umuhimu wa watalaam wa usafiri wa anga katika nchi za
Afrika Mashariki kupatiwa mafunzo ya kutosha kuimarisha ujuzi na uwezo wa utendaji kumudu majukumu yao.
Awali
wajumbe zaidi ya 70 wa kamati ya Kuwezesha Usafiri wa Anga katika nchi za
Afrika Mashariki walitembelea kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume
(AAKIA) ili kujionea miundombinu na huduma
zinazotolewa katika kiwanja hicho cha ndege.
Wajumbe
hao wa kamati ya Afrika Mashariki kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Mwenyeji Tanzania hukutana mara
mbili kwa mwaka kwa lengo la kujadili
ubora wa utoaji huduma za usafiri
anga kwa abiria na mizigo .
Kamati hiyo hujadili changamoto na
kupendekeza suluhu za kuboresha sekta hiyo kwa lengo la kuwezesha sekta hii kutoa
mchango katika kukuza uchumi wa nchi wanachama.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akizungumza katika mkutano wa kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki Unaofanyika Zanzibar.
Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akifungua rasmi mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki uliofanyika Zanzibar leo.
Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akiwapongeza Wajumbe waliostaafu wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki kwa mchango wao katika Kamati.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki walipotembelea Kikosi cha Zimamoto katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA)
Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amani Karume,(Kulia) akishiriki Mkutano wa 41 wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...