Serikali ya awamu ya tano yadhamiria kujenga mahakama za mwanzo katika kila kata nchini ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe ameyasema hayo alipotembelea ujenzi wa Mahakama ya kisasa ya Wilaya Kigamboni ambayo inajengwa kwa kutumia teknolojia ya Moladi ambapo teknolojia hii inapunguza muda na gharama za ujenzi. Mahakama ya Wilaya ya Kigamboni inagharimu kiasi cha shilingi milioni 572 na inatarajiwa kukamilika ifikapo Februari 2017.
Waziri Mwakyembe amesema Wizara ya Mambo ya Katiba na sheria moja ya kipaumbele chake ni kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi hivyo huduma za kimahakama zitaendelea kuboreshwa ilim kusogeza huduma kwa wananchi.
Waziri aliongeza kuwa Sheria ya Msaada wa Kisheria itakapoanza kutumika itasaidia wananchi hasa wasio na uwezo kupata haki zao kupitia wasaidizi wa kisheria.
“Sheria ya Msaada wa Kisheria itakapoanza kutumika itasaidia wananchi hasa wasio na uwezo kupata haki zao kupitia wasaidizi wa kisheria ambao watapatiwa mafunzo rasmi’. Waziri alisema.
Akiishukuru Serikali Mbunge wa Kigamboni Mhe. Faustine Ndugulile amesema anaishukuru Serikali kwa kujenga Mahakama ya kisasa Kigamboni na kusogeza huduma kwa wananchi na pia ameipongeza Serikali kwa kuanzisha sherian ya Msaada wa Kisheria ambayo itasaidia sana wananchi wa kipato cha chini.
Aidha, Mhe. Ndugulile ameomba changamoto za ucheleweshwaji wa kesi Mahakamani na rushwa ziweze kutafutiwa ufumbuzi maana ni kero kwa wananchi.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akisisitiza jambo wakati akiangalia mchoro wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kigamboni alipotembelea leo (16/12/2016) ili kujionea ujenzi wa Mahakama hiyo ambao unatumia teknolojia ya Moladi.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akiangalia mchoro wa jengo la Mahakama ya Wilaya Kigamboni.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (mwenye miwani) akionyeshwa vyumba mbalimbali vitakavyotumika katika jengo la mahakama ya wilaya kigamboni ikiwemo mahabusu na vyumba vya mahakama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...