Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye, (wapili kushoto), akipokea fomu ya kujiunga na uanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bw. Adam Mayingu, wakati wa Mkutano Mkuu wa Mtandao wa Bolggers Tanzania, (TBN), uliomalizika jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa TBN, Bw. Joachim Mushi.
Waziri Nape, akipokea kadi yake ya kujiunga na Mfuko huo kutoka kwa Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi.


NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Moses Nnauye, amejiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF na kuusifu kwa huduma zake za haraka.

Waziri Nape, amejiunga muda mfupi baada ya kufunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), kwenye jingo la kitega uchumi la Jubilee Towers linalomilikiwa na Mfuko huo jana.

Aidha wajumbe wa mkutano huo ambao ni bloggers kutoka kila pembe ya nchi wapatao 100 nao pia walijiunga na Mfuko huo kupitia uchangiaji wa Hiari yaani PSS.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kadi yake ya uanachama iliyotengenezwa chini ya dakika 15, Waziri Nape alisema, “Aise, kitambulisho changu tayari? Hongereni sana kwa huduma za haraka. Mimi sikujua kama mnafanya kazi kwa kasi yanamna hii,” alisema Mh. Nape wakati akikabidhiwa kadi hiyo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi ofisini kwake.

Tangu kujaza fomu, kupiga picha na kukabidhiwa kitambulisho hicho, Waziri alitumia kiasi cha dakika 25 tu, ikiwa ni muda mfupi baada ya kufunga mkutano huo.

Nao wanachama wa Mtandao wa Bloggers Tanzania, (TBN), waliokuwa wakishiriki mkutano huo, wamejiungana PSPF, baada ya kupatiwa maelezo ya kina kuhusu umuhimu wa kujiunga na Mfuko, kutkana na manufaa mengi ukiachilia mbali kujiwekea akiba.

“Ukiwa Mwanachama wa Mfuko, moja ya faida kubwa ni kujipatia bima ya Afya, itakayokusaidia wewe na familia yako, nikiwa na maana ya mke/mume na watoto,” alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdyul Njaidi katika mada yake aliyoitoa kwa washiriki kuhusu kazi za Mfuko huo.
Waziri Nape, akijaza fomu hiyo, kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu na kulia ni Bw. Abdul Njaidi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...