Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Milao (kulia), akifungua warsha (mafunzo) ya siku tatu kwa wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, yaliyoanza hii leo katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mara iliyopo Musoma Mjini. Wengine ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini, Bi.Joyce Fisso(katikati) pamoja na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto).

Warsha hiyo imeandaliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Bodi ya Filamu nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wanatasnia ya filamu na maigizo ili kuzalisha kazi zenye ubora (maudhui) na kuboresha soko la ndani na nje ya nchini, kama kaulimbiu isemavyo, "Filamu ni Uchumi, Filamu ni Ajira".
Tayari warsha ya aina hiyo imefanika mikoa ya Morogoro na Mwanza ambapo pia itaendelea kufanika katika mikoa mingine nchini ikiwa pia ni utekelezaji wa kauli ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nnauye, kuhakikisha wizara hiyo inafikisha huduma zake mikoani badala ya Dar es salaam pekee.
Wanatasnia ya Filamu na Maigizo mkoani Mara, wakifuatilia mafunzo kutoka kwa Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaa, idara ya Sanaa, Richard Ndunguru.

Zaidi ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya filamu na maigizo kutoka  Bodi ya Filamu nchini. Pia wawakilishi kutoka maeneo jirani ikiwemo Simiyu wamehudhuria mafunzo hayo.


Zaidi ya wanatasnia 200 wa Filamu na Maigizo mkoani Mara wamepatiwa mafunzo ya filamu na maigizo kutoka  Bodi ya Filamu nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...