Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania,
Benoit Janin (wa tatu kulia), akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo
wakifanya usafi eneo la Forodhani mjini Zanzibar mwishoni mwa wiki ikiwa ni
sehemu ya juhudi za Zantel kujitolea kufanya kazi za jamii.. Mara baada ya
kufanya usafi, Zantel ilikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi vyenye
thamani ya zaidi ya shs milioni 3 kwa uongozi wa serikali ya mji
huo kama sehemu ya kurudisha sehemu ya mapato yao kwa
jamii wanayofanya nayo biashara.
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis
(kulia) akikabidhi vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa mwakilishi wa manispaa, Khamis Msabah vilivyotolewa na Zantel ikiwa ni
sehemu ya juhudi zao kufanya kazi za kijamii na kurudisha sehemu ya faida
waipatayo kwa jamii. Awali ofisa mtendaji wa kampuni hiyo akiwa na baadhi ya
wafanyakazi walifanya usafi katika eneo la Forodhani, visiwani humo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zantel Tanzania,
Benoit Janin (kulia), akitoa zawadi ya vocha kwa wateja waliokuwa wakihudumiwa
katika kituo cha huduma kwa wateja cha Vuga mjini Zanzibar ikiwa ni moja ya
kuonyesha shukrani kwa wateja wao. Ofisa huyo pamoja na baadhi ya wafanyakazi
wa kampuni hiyo walikuwa visiwani humo mwishoni mwa wiki ambapo walitembelea
wateja na wakala wao na baadae kufanya shughuli za kusafisha mazingira eneo la
Forodhani na pia kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi kwa uongozi wa manispaa ya
mji humo ikiwa ni mwendelezo wa shughuli a kuhudumia kijamii. Kulia kwake ni
Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Khamis Baucha.
Baadhi ya wafanyakazi wa Zantel
wakishiriki zoezi la kufanya usafi eneo la Forodhani mjini Zanzibar ikiwa ni
sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kujitolea kufanya kazi za kijamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...