
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi,Mh.Saleh Mbwana Mhando leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua shughuli mbalimbali za uvuvi wa samaki aina ya Sangara na Dagaa katika mwambao wa ziwa Tanganyika mkoani humo.Dc Mhando amesema kuwa ziara hiyo imelenga kuangalia fursa mbalimbali zilizopo na kuwawezesha wavuvi hao wadogo wadogo.Pichani Dc Mhando (pili kulia) akipata maelezo mafupi kuhusiana na mradi huo wa kukausha dagaa pembezoni mwa ziwa Tanganyika,mkoani Katavi.

Samaki aina Sangala kama aonekanavyo pichani mara baada kuvuliwa kwenye ziwa Tanganyika.

Mmoja wa akina mama wanaojishughulisha na ukaushaji wa dagaa pembezoni mwa ziwa Tanganyika,akimuelezea Dc Mhando changamoto mbalimbali wazipatazo kuhusiana na suala zima la soko na usafirishaji
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...