Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ

Klabu ya golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania imetuma salam za rambirambi kwa Mhariri Mtendaji wa Magazeti  ya Uhuru, Burudani na Mzalendo kufuatia kifo cha Mwandishi wake wa habari za michezo Amina Athumani.

Akizungumza katika Kikao cha maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya Miaka 10 ya klabu hiyo mahiri ya golf nchini Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Michael Luwongo alisema kifo hicho si pigo kwa kampuni yake pekee bali na Klabu ya Lugalo ambayo  amekuwa akijitokeza katika mashindano Mbali mbali yaliyoandaliwa na klabu hiyo.

“Niseme ukweli tangu nimekuwa mwenyekiti miongoni mwa Waandishi waliozoeleka kuandika michezo mingine hasa soka walianza kutupia macho na Golf ni pamoja na  Amina ambaye alikuwa hakosi katika mashindano ya Golf”, Alisema  Brigedia Jenerali Luwongo.

Katika Salamu hizo ambazo pia zimekwenda kwa  Mwenyekiti wa wa Chama cha Waandishi wa habari za Michezo (TASWA) Juma Pinto  ambapo Brigedia Jenerali Luwongo  alisema hakika kifo hicho kimepunguza idadi ya waandishi wa habari wanaoangazia mchezo huo.

Briigedia Jenerali Luwongo aliongeza kuwa ni kipindi kigumu kwa familia ndugu na marafiki hivyo amewataka kuwa na moyo wa subira katika kipindi hichi kigumu kwa wanamichezo.

“Binafsi naweza kusema shujaa aliyefia katika mapambano lakini hatuwezi kupingana na mipango ya mungu nilipokea kwa masikitiko  taarifa ya kifo chake tasnia na Uhuru publication imepoteza mwanahabari mahiri”Alisema Brigedia Jenerali Luwongo.

Taarifa zinasema Amina Alifariki Dunia  Jumapili January 15,2017 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mnazi mmoja Zanzinzibar alikokwenda kwa ajili ya kuripoti michuano ya Mapinduzi.

Amina alijifungua mtoto ambaye alifariki muda mfupi baada ya kuzaliwa  na mpaka mauti yanamkuta alikuwa mwandishi wa michezo wa kampuni ya Uhuru publications .

Mungu ailaze roho ya marehemu Amina Athumani anayetarajiwa kuzikwa mkoani Tanga mahala pema panapostahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...