Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Mtabiri na mnajimu maarufu Tanzania, Malim Hassan Yahya Hussein ametabiri makubwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais John Pombe Magufuli huku akitaja moja ya chama cha upinzani kufa.
Yahya amesema kuwa anatabiri Chama cha Mapinduzi kushika hatamu katika chaguzi mbalimbali za mwaka huu huku moja ya chama kikuu cha upinzani kufa na viongozi waliotoka chama tawala kurudi huku viongozi wa dini na kisiasa kukumbwa na kashfa za ngono na ulevi.
“natabiri Rais John Pombe Magufuli kupata nishani ya juu ya Dunia kutoka kwa rais wa moja ya mataifa makubwa kutokana na uongozi wake” amesema Malim Yahya.
Aidha ametabiri kuwa katika kipindi cha mwaka 2017 viongozi kadhaa wa mataifa mbalimbali duniani watatoa matamshi ya ajabu yatakayowashangaza raia na wananchi wa nchi zao kiasi cha kusababisha kuanguka au kuuwawa kwa viongozi hao.
Pia amesema kuwa katika utabiri mwingine kuwa kutakuwepo kwa ajali nyingi zitakazo wakuta wanasiasa watawala na viongozi wa dini.
Alimaliza kwa kutoa ushauri kuwa vifo na maafa vinaweza visitokee iwapo watu wataacha rabsha na uharaka wa kufanya mambo kama nyota ya mwaka 2017 inavyosema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...