Na Bashir Yakub.
1.WOSIA NININI.
Wosia ni matakwa ya mtu ambayo angependa yatekelezwe baada ya kifo chake. Yanaweza kuwa matakwa kuhusu mali, maziko, madeni, watoto,mke/wake n.k.
2. AINA ZA WOSIA.
Tunao wosia wa maandishi na wosia wa maneno, lakini pia tunaweza kupata aina za wosia kutokana na sheria mbalimbali zinazotumika kugawa mali za mirathi kama ifuatavyo :
( i ) Wosia wa Kiislamu. Ni wosia ambao misingi yake itakuwa ni kutokana na Quran Tukufu, Sunna na Hadith za mtume Muhammad S.AW. Aina hii ya wosia ni maalum kwa mtu aliyeishi maisha ya kiislam(muislam).
( ii ) Wosia wa kikristo. Ni aina ya wosia ambao misingi yake imejengwa katika misingi ya Sheria ya Urithi ya India ( The Indian Succession Act , 1865) . Sheria hii kwa jina hilo hilo la Sheria ya Urithi ya India ndiyo hutumika hapa Tanzania kwa mtu aliyeishi maisha ya kikiristo(mkristo).
( iii ) Wosia wa kimila . Misingi ya wosia huu imejengwa katika Azimio la Sheria za Kimila ( The Local Customary Law Declaration Order G.N. No. 279 of 1963) . Wosia huu hutumika kwa watu walioshi kimila.
3. NI WOSIA UPI UANDIKE KATI YA HIZI.
Niseme mapema tu kuwa unapoandika wosia hakikisha unaandika kwa kufuata misingi ya mfumo wa maisha yako ( dini yako). Hili si hiari ni lazima.
Unapofanya kosa la kuandika wosia bila kufuata misingi ya sheria husika kwa kujua au kutokujua basi wosia huo utakuwa ni batili.
Unaweza kudhani umeandika wosia na kuamini kuwa mambo yote sasa yako vizuri lakini kumbe hujaandika wosia.
4. JE WOSIA NI UTASHI WA MTU ?.
Ndio, wosia ni utashi wa mtu lakini utashi wenye mipaka. Wengi hudhani kwakuwa wosia ni utashi na mali ni zako basi unaweza kufanya/kugawa unavyotaka . Kwa wanaojua hivi mawazo yao sio sahihi.
Pamoja na wosia kuwa utashi ni lazima mgao pamoja na kanuni za uandaaji wake zirandane na sheria husika. Kama we ni muislamu lazima ugawe kama sheria na kanuni za kiislamu zinavyosema, kama ni mkristo au mtu wa mila ni lazima ufuate sheria inayokuhusu inavyosema. Sheria zenyewe ni hizi hapo juu zilizoelezwa katika 2.
Nirudie tena kuwa hautagawa wala kuandika unavyotaka isipokuwa utagawa na kuandika kama sheria inayokuhusu inavyotaka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...