Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa tatu kushoto) akimkabidhi nahodha wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), Ally Rabi (wa tatu kulia) fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es Salaam (CBE), wakiwa katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Biashara Kanda ya Dar es salaam wa Kampuni ya Simu nchini Tanzania (TTCL), Jane Mwakalebela (wa nne kushoto) mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya fedha shs 600,000/- pamoja na laini za TTCL za 4G LTE zenye muda wa maongezi wa simu na intaneti (10GB) kwa muda wa mwezi mmoja baada ya kuibuka washindi wa Mashindano ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer'. CBE ilikifunga Chuo cha Ardhi mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika Ufukwe wa Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Mapambano mbalimbali ya mechi za Mashindano ya Soka la Ufukweni 'TTCL Inter College Beach Soccer' yakiendelea.
Pongezi sana kwa TTCL ambayo inakuwa kama inatoka kwenye kiza kirefu kuhusiana na maswala ya masoko ,kudhamini matukio kama haya kunaleta ukaribu kati Yao na Jamii ,TTCL isiishie hapa izidi kujichanganya zaidi kwenye jamii na hii itawaletea return nzuri sana huko tuendako!!
ReplyDelete