Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi (kulia) akisikiliza kilio cha wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya alipotembelea kujionea na kusikiliza changamoto za huduma za afya katika jimbo lake ili kuzitafutia ufumbuzi na kuboresha huduma hiyo.
Na Fredy Mgunda, Iringa
MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi alifanya ziara ya kuzitembelea zahati,vituo vya afya na hospitali za jimbo hilo kwa lengo la kujionea changamoto za kiafya.
Akiwa katika ziara hiyo alikumbana na changamoto ya kukosekana kwa umeme katika baadhi zahati za jimbo hilo na kuahidi kulipeleka tatizo hilo bungeni ili litafutiwe ufumbuzi mapema.
Akizungumza na blog hii Chumi alisema tatizo la umeme katika vituo na zahati ni kubwa hivyo inahitajika nguvu ya ziada kutatua tatizo la umeme ili kuboresha afya za wananchi wake pamoja na huduma ya mama na mtoto.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...