Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii mapema leo, inaeleza kuwa chombo (Jahazi) cha nahodha Badru Said kilichoondoka Mkoani Tanga jana usiku kuelekea wete Kisiwani Pemba kimepatwa na dhoruba ya bahari na kuzama umbali mfupi kutokea bandari ya Tanga, na kudaiwa kuwa watu zaidi ya 13 wamepoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa na kupoteza fahamu na baadae kuwahishwa hospitali ya Rufaa ya Bombo Mkoani Tanga kwa matibabu ya haraka.
Kwa mujibu wa mmoja wa abiria katika chombo hicho, Mahfoudh Khamis ambaye yupo katika hospitali ya Bombo akipatiwa matibabu, amesema kuwa jumla ya maiti 13 zilipatikana akiwemo Nahodha mwenyewe wa Chombo hicho, Badru Said na majeruhi zaidi ya 30 wameokolewa na kulazwa hospitalini hapo.
Inaelezwa kuwa kuna wengine waliokoka na kurudi makwao ambao idadi yao haikufahamika kwa haraka, Wengi waliokuwamo kwenye chombo hicho inadaiwa ni wanawake na watoto ambao walikuwa wanarudi likizo zao za Mwezi Disemba.
Mungu azilaze peponi roho za Marehemu wote na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.
Amin .
Aaamy mungu awajaalie safari yenye kheri
ReplyDelete