Na Mwandishi wetu
Muogeleaji chipukizi wa
Tanzania Collins Saliboko (pichani) ambaye ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya
Jumuiya ya Madola ya Vijana ameahidi kuipeperusha vyema bendera ya nchi na kuweka historia katika mashindano hayo kwa
mara ya kwanza.
Mbali ya Collins ambaye
anashindana kwa upande wa wanaume, msichana Celina Itatiro ataiwakilisha nchi
kwa upande wa wanawake katika mashindano hayo yaliyopangwa kufanyika nchini
Bahamas kuanzia Julai 18 mpaka 23 kenye mji wa Nassau.
Collins ambaye kwa sasa
anasoma Chuo cha St Felix, Uingereza, amesema kuwa ameanza mazoezi kwa ajili ya
mashindano hayo chini ya kocha wake, Sue Purchase amesema kuwa amepania kufanya
kile ambacho watanzania wengi hawatakitarajia kupitia mchezo wa kuogelea ambao
kwa sasa unakuja juu kwa kasi.
Alisema kuwa atatumia
pia mazoezi ya timu ya kuogelea ya chuo chao kama sehemu ya maandalizi, kabla
ya kujiunga na kambi ya timu ya Taifa ambayo itatangazwa hapo baadaye.
“Naahidi kuitendea haki
nafasi hii. Na hii inatokana na juhudi zangu katika mchezo wa kuogelea. Matokeo
yangu bora ndiyo yamenipa nafasi hii. Nnaona mwanga katika mchezo wa kuogelea
na ninaahidi kufanya vyema.
“Mazoezi ya hapa St
Felix ni mazuri sana. Hii inatokana na kuwepo vifaa bora na walimu wazuri. Hapa
pia kuna ushindani mkubwa na hivi juzi juzi tu nilishinda nafasi ya
pili kwenye mashindano ya huku Uingereza, ni matokeo mazuri na ninaahdi kufanya
vyema zaidi,” alisema Collins kwa njia ya simu.
Alisema kuwa mpaka sasa
ameshiriki katika mashindano mengi ya ngazi ya chuo na kupata matokeo mazuri.
“Mashidano haya ya Chuo ni sehemu ya maandalizi yangu, naishi hapa chuoni, kila
Napata muda mwingi wa kujifunza, Mwalimu wangu, Sue ni mkali na kwa sasa anajua
jukumu langu la kitaifa, hivyo ameongeza ‘dozi’ ya mazoezi,” alisema.
Katibu Mku wa Chama Cha
kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhan Namkoveka alisema kuwa kazi iliyopo sasa ni
kwa makocha kuwaandaa wachezaji katika matukio watakaoshiriki ili kuweza
kufanya vizuri.
Namkoveka alisema kuwa
mbali ya kusaka medali, lengo kuu la chama kwa wachezaji hao ni kupunguza muda
wao ili baadae waweze kufikia muda unaotakiwa na Shirikisho la
mchezo wa kuogelea duniani, (FINA) kiwango cha muda B au A.
Mashindano ya
Jumuiya ya Madola haya yatakuwa ya sita baada ya kuanzishwa kwake mwaka 2000 ambapo
vijana 1000 wenye umri wa
miaka kuazia maika 14 hadi 18 wanatarajiwa kushindana katika michezo
mbalimbali.
Muogeleaji wa Tanzania Celina Itatiro akichupa kwenye mashindano ya Afrika Kusini
Collins Saliboko akichapa maji St Felix College, Uingereza
Celina Itatiro (Mwenye kofia ya orange) akiogelea huku akiwa na kikombe cha maji kwenye paji la uso
Collins Saliboko (wa kwanza kulia) akiwa na waogeleaji wa Tanzania wanao soma St Felix College; Aliasgar Karimjee na Sonia Tumiotto mara baada ya kutwa medali katika mashindano ya chuo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...