Lusubilo Joel Ded Kakonko
Na Judith Mhina –MAELEZO
Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko yafaulisha wanafunzi 743 kati ya watahiniwa 784 na kushika nafasi ya Tatu Kitaifa kati ya Halmashauri 178hapaTanzania.
Katika mahojiano maalum na Idara ya Habari MAELEZO Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kakonko Bw Lusubilo Joel Mwakabibi amesema: “Shule za serikali zimeanza kurudisha heshima ya kufaulu kama ilivyokuwa miaka ya 1970 na 1980, mara baada ya matokeo ya kidato cha Nne mapema mwezi huu”.
Mwakabibi ameeleza kuwa Halmashauri hiyo inajumla ya shule           za sekondari 14, kati ya hizo 11 ni za Serikali na 3   za binafsi. Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu
Yanaonesha daraja  la  kwanza shule za binafsi ni 10,  pili  35, tatu 40, nne 41 na zilizopata ziro ni 13. Kwa upande wa Shule za Serikali daraja la kwanza 6, pili 47, tatu 149, nne 400 na ziro 38.
 “Siri ya mafanikio yetu ni usimamizi wa karibu na ufuatiliaji shuleni, umoja na mshikamano kati ya Walimu, wazazi, Viongozi wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa wilaya; walimu wetu tupo pamoja nao, tunawatia moyo katika kazi ya kufundisha”. Anafafanua Mkurugenzi huyo.
Aidha, Mkurugenzi Mwakabibi amesema mwaka 2016 Halmashauri imeshika na fasiyatatu, Kitaifa katika Halmashauri 178 Tanzania, kwani matokeo ya kidato cha Nne na Pili mwaka 2015, Halmashauri yetu, ilikuwa ya kwanza kitaifa na kuzawadiwa ngao ya ushindi toka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

 Hata hivyo ameeleza kuwa mikakati ya Halmashauri yake ni kurudi namba moja, lengo likiwa ni kuhakikisha wanafunzi wote watakao sajiliwa kufanya mtihani wa kufaulu kwa viwango vya juu na kufuta kabisa aibu ya kufeli..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...