JPCC kati ya Tanzania na Malawi ni chachu ya kuimarisha mahusiano
Wajumbe wanaoshiriki katika Kikao cha 4 cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kilichofunguliwa leo jijini Lilongwe, Malawi wamehimizwa katika majadiliano yao ya siku tatu kubuni mkakati utakaowezesha kutatua changamoto zinazojitokeza kutokana na muingiliano mkubwa wa ngazi mbalimbali za ushirikiano baina ya wananchi wa mataifa hayo mawili.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Wataalam, Balozi Ramadhan Mwinyi ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipokuwa anasoma hotuba ya ufunguzi.
"Kama mnavyofahamu kunapokuwa na maingiliano makubwa ya wananchi wa nchi mbili kama zilivyo nchi zetu, changamoto haziwezi kukosa kujitokeza. Hivyo ni jukumu letu sisi wataalamu kubuni mkakati wa kuhakikisha kuwa changamoto hizo zinashughulikiwa haraka iwezekanavyo".
Balozi Mwinyi alieleza kuwa kikao hicho ni fursa nzuri kwa Serikali za Tanzania na Malawi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya nchi zao katika maeneo tofauti ikiwemo uchumi, uwekezaji, biashara, kutunza mazingira, elimu, Tehama, kilimo, uhamiaji, uchukuzi na masuala ya ulinzi na usalama, Hivyo alihimiza wajumbe wa pande zote mbili kuwa wabunifu katika majadiliano yao ili watoke na mipango inayotekelezeka kwa kuwa wananchi wanachohitaji ni maendeleo na sio mikakati inayoishia katika makabrasha.
Aidha, Balozi Mwinyi aliekeza kuwa watu wengi walistaajabu kusikia ujumbe wa Tanzania unakuja Malawi kushiriki kikao hiki kama walivyostaajabu kuona Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya mazungumzo hivi karibuni na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia. Alisema hakuna cha kustaajabisha hapo, isipokuwa ifahamike lengo kuu la pande zote mbili ni kuona uhusiano kati ya Tanzania na Malawi unaimarishwa na kwamba mkutano huo ni ushahidi kuwa nchi hizi mbili zipo karibu zaidi kuliko hapo awali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi na Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi, Dkt. Kalitso Kabambe akisoma hotuba ya iufunguzi na ukaribisho.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi akisoma houtuba ya ufunguzi wa kikao cha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Dkt. Dalitso Kabambe. Kikao hicho kinafanyika Lilongwe, Malawi kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 03 Februari 2017.
Wajumbe wa Tanzania wakisikiliza hotuba za Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Amos Makalla, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Suleiman Salehe na Kaimu Mkurugenzi kutoka Mamlka ya Viwanja vya Ndege.
Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Ali Ubwa na mjumbe mwingine ambaye jina lake halikupatikana.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...