Hiyo Story inyayozagaa mitandaoni kupitia link hio hapo juu ni Uzushi na iipuuzeni.  Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi yuko salama nyumbani kwake, na jana alikuwa kwenye hafla hiyo hapo chini. Jioni hii ataungana na Jumuiya ya Mabalozi pamoja na wadau wengine katika kusherehekea Siku ya Taifa ya Kuwait iliyoandaliwa na Balozi wa nchi hiyo hapa Dar es Salaam. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie afya na siha njema na umri mrefu - Amin

Dkt Abdullah H. MAKAME_

 Katibu wa Rais Msaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi.
  Rais Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitembelea  mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) yaliyofikia kilele jana tarehe 22/02/2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Shirika la "Pressures Blood" Tanzania Padre Chesco Msanga, akimkabidhi zawadi ya picha Rais Mstaafu Mzee Ally  Hassan Mwinyi kama kumbukumbu alipoifungua Hospital ya St. Gaspar Itigi inayoendeshwa na shirika hilo

Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC). 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...