Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala akitangaza kikosi cha watu nane kutoka nje ya halmashauri ya Jiji kinachojumuisha watalaam wa ardhi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, halmashauri Mbeya, Mkuu wa Wilaya, wanasheria na vyombo vya Dola.
amesema kikosi kazi kitaanza kwa awamu ya kwanza ambapo kitashughulikia migogoro ya ardhi Kata ITEZI na MWAKIBETE.
Amekipa kikosi kazi hicho muda wa siku 14 kushughulikia migogoro katika kata hizo mbili na watoe ushauri wa namna ya kuimaliza migogogoro iliyopo.
Amebainisha kuwa migogoro mingi katika jiji la Mbeya inakutokana na kutolipa fidia, umilikishaji watu zaidi ya mmoja katika kiwanja kimoja na Baadhi ya wawekezaji kutoendeleza maeneo yao kwa muda mrefu
Amefanikiwa kumaliza mvutano wa umiliki wa soko kati ya CCM na serikali ya mtaa na kata. Kwa mujibu wa hati za kiwanja CCM ni wamiliki halali kwa kuwa na hati Bambi 81 BB
Mkuu wa Mkoa huyo amepokea kero mbalimbali kutoka kwa wananchi kuhusiana na Mgogoro wa wananchi na wamiliki wa ardhi maeneo ya viwanda.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makala akitoa maagizo wakati alipotembelea sehemu mbalimbali zenye migogoro ya ardhi jijini humo
Wananchi wakitoa kero zao za ardhi kwa Mkuu wa Mkoa wa mbeya kuhusiana na migogoro ya ardhi.
Wananchi wakitoa kero zao za ardhi kwa Mkuu wa Mkoa wa mbeya kuhusiana na migogoro ya ardhi.
Wananchi wakitoa kero zao za ardhi kwa Mkuu wa Mkoa wa mbeya kuhusiana na migogoro ya ardhi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...