Na Eliphace Marwa -Maelezo

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha safari ya kwenda nchini India kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Dkt. Mrema ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu uteuzi uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kuwateua wajumbe wawili wa bodi hiyo.

“Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais Magufuli , Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Wizara ya Afya na Ikulu, kwa kunipeleka nchini India kufanyiwa uchunguzi wa afya yangu na kupatiwa matibabu na sasa afya yangu imeimarika na niko tayari kutekeleza majukumu yangu”, alisema Dkt. Mrema.

Akizungumzia uteuzi uliofanywa na Waziri Nchemba, Mrema amesema kuwa toka alivyoteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Bodi hiyo haikukaa vikao kutokana na baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo kumaliza muda wao.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza tarehe ya uzinduzi wa bodi mpya ya parole taifa tarehe 3 na 4 Machi 2017 mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Msaidizi wake Bw. Clemence Munisi na kulia ni Mkewe Bi. Rose Augustino Mrema.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema (katikati mwenye kofia) wakati akitangaza tarehe ya uzinduzi wa bodi mpya ya parole taifa tarehe 3 na 4 Machi 2017 mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...