Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi, ameipongeza Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kutimiza miaka 25 tangu ilipoanzishwa mwaka 1992.  Akiongea katika maadhimisho hayo, Mzee Mwinyi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitambua na kuthamini mchango wa makanisa na Taasisi za dini katika kuboresha huduma za Jamii.

“Nimefarijika sana kwa kupata taarifa kuwa hadi kufikia Septemba 2016, hospitali za Kanisa 87 na vituo vya afya 45, vimeingia Mkataba na Serikali katika kutoa huduma za afya”, alisema Rais Mstaafu Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mzee Mwinyi aliongeza kuwa kwa upande wake yeye amekuwa mstari wa mbele kwa kuwaasa ndugu jamaa na marafiki zake na Watanzania wote kwa ujumla, kutumia huduma zitolewazo na hospitali za kanisa kwa kuwa wanatoa huduma bora, kwa kuzingatia upendo

“ Ikiwa mnaona kazi zinawazidia na mnafikia sehemu mnanung’unika kwa kuzidiwa na kazi nyingi, basi ningesema mgomvi wenu ni mie. Maana nawaambia ndugu na Watanzania wenzangu, kuwa huduma nzuri za afya zinapatikana katika hospitali za Kanisa, kwa kuwa unahudumiwa kwa upendo pamoja na tabasamu,” aliongeza Rais Mstaafu, Mwinyi.

 Rais Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitembelea  mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) yaliyofikia kilele siku ya tar 22/02/2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
 Mkuu wa Shirika la "Pressures Blood" Tanzania Padre Chesco Msanga, akimkabidhi zawadi ya picha Rais Mstaafu Mzee Mwinyi kama kumbukumbu alipoifungua Hospital ya St. Gaspar Itigi inayoendeshwa na shirika hilo
 Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC).
Mzee Mwinyi akitoa Cheti kwa  Profesa Costa Mahalu, moja ya watu waliyotoa msaada mkubwa wa masuala ya Sheria kipindi Tume hiyo ilipokuwa inaanzishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...