Kamati ya Mpito TZUK kwa masikitiko makubwa imepokea taarifa za msiba wa Baba mzazi wa Ndugu yetu, Mtanzania na mwanajumuiya mwenzetu Ndugu Frank Mlay (Daddy Big). Marehemu Mzee  Gasper Mlay amefariki tarehe 06/02/2017, Moshi TANZANIA.
Taratibu za msiba zinaendelea kufanywa nyumbani kwa marehemu Tanzania na mfiwa amesafiri kuelekea Tanzania, ili kuwahi mazishi. Tunaomba kumsaidia mwenzetu aweze kumpumzisha mzazi wake kwa amani , na kumuombea safari njema na Mungu ampe Faraja katika kipindi hiki kigumu. 
Wanajumuiya, Watanzania, Ndugu, Jamaa, na marafiki tunawaomba sana tujitoe kwa hali na mali kumfariji mwenzetu katika kipindi hiki kigumu na cha majonzi.
Michango yote ielekezwe moja kwa moja kwa Kutumia akaunti ifuatayo;

Account name -  D A Wilson
Account No. 40416290
Sort Code.  20 - 98 - 57
Barclays Bank.
Kamati ya Mpito TZUK Itaendelea kuwapa taarifa zaidi za msiba na mahitaji nyumbani Tanzania, Mungu awabariki kwa kujitoa kwenu kuwafariji na kuwa pamoja na familia ya Marehemu.
Tunawaomba sana Watanzania UK na Northern Ireland tuonyeshe mshikamano kwa Upendo na Umoja kwa kumchangia Mwenzetu kwa hali na Mali tafadhali weka jina lako hapa na kiasi ulichochangia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...