Viongozi wa kata na mitaa wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,wametakiwa kutoka nje ya ofisi zao ili kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Akizungumza na wananchi wa kata ya Kinondoni katika ziara yake ya siku kumi, mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amesema viongozi wote wakitaifa akiwemo raisi, waziri mkuu na mawaziri wanafanya ziara za kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Hatahivyo mkuu huyo wa wilaya amewataka viongozi wa kata na mitaa kuwa wabunifu na kuwashirikisha wadau ili kuweza kutatua changamoto ndogondogo tofauti na kuzipeleka kwa ofisi ya mkuu wa wilaya.

Aidha amesema serekali ya awamu ya tano imejipanga kikamilifu kutatua kero za wananchi nakutekeleza kikamalifu ilani ya chama cha mapinduzi kwa mwaka 2015/2020.


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akitoka katika ofisi ya mtendaji wa Kata ya Kinondoni akielekekea kukagua miradi mbambali na Kinondoni leo hii katika Ziara yake
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ally hapi akiwashukuru wafanya biashara katika soko la mtambani lililo kinondo ni Jijini Dar es salaam leo hii.
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni wilaya ya Kinondoni Ally Hapi Akizungumza na viongozi wa Kata na mitaa wilaya ya Kinondoni Jijini dar es salaam leo hii katika Ziara yake ya kukagua miradi mbambali na kusikiliza kero za wakazi wa Kinondoni Pembeni Kushoto ni Diwani wa Kata ya Kinondoni Mustapha Muro 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...