WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa asimamie zoezi la upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na Magereza kote nchini na kuhakikisha yanawekewa mipaka. 
Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Februari 13, 2017) katika kikao baina ya Kamishna huyo mpya na Maafisa Magereza wa Mikoa yote na maafisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma.
“Magereza yetu mengi yako kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na maeneo ya Magereza. Lazima tupime maeneo yote na kuyawekea alama mipakani ili kubainisha maeneo yetu,” amesisitiza.
Mbali ya maeneo ya Magereza, Waziri Mkuu amesema, jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo amesema imechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi hilo.
“Natambua kuwa jeshi hili lina mashamba makubwa lakini nayo pia hayajapimwa. Kila RPO ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapima ardhi kutoka kwenye Halmashauri zenu na mhakikishe kuwa maeneo hayo yanapatiwa hati,” amesema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiongoza kikao kati yake na Maofisa wa Magereza kutoka makao Makuu ya Magereza , pamoja na Makamanda wa Magereza wa Mikoa yote nchini, ofisini kwake mjini Dodoma Februari 13, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Watalaamu na Wasimamizi wa Mkiradi ya Jeshi la Mgereza, baada ya kikao chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza na Wakuu wa Magereza wa Mikoa kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma Februari 13,2017. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Kamishina Jenerali wa Magereza, Dr Juma Malewa baada ya kikao chake na Maofisa wa Magereza kutoka Makao ya Magereza kilichofanyika Ofisini kwake mjini Dodoma Februari 13,2017. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani Meja Jenerali Projest Rwegasira.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...