Timu ya kata ya Tengelea, Tengelea FC imefunzu kuingia katika fainali ya Ulega Cap baada ya kuifunga Timu ya Mwandege FC bao 1 – 0 katika mcheezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana .
Bao la timu ya Tengelea lilipatikana katika kipindi cha pili kupitia mchezaji wao Andew Joseph aliyepokea cross ambayo ndio ilipa ushindi timu hiyo.
Timu ya kata ya Tengelea, itaingia fainali kwa kukipiga na timu ya Kisiju na mechi itanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya Mwandege FC na Lukanga FC.
Mgeni rasmi katika fainali za Ulega CUP ni Waziri Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa, Nape Nnauye.
Akizungumza na waandishi wa habari muandaji wa mashindano hayo Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega amesema kuwa mashindano yameibua vipaji ya vipya.
Amesema kuwa inahitaji uwekezaji katika michezo kutokana na vijana kuonyesha vipaji vyao ambavyo vinatakiwa kuendelezwa.
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Tengelea iliyopata ushindi wa kuingia fainali ya Ulega CUP katika mchezo uliochezwa jana katika viwanja vya shule ya Mkuranga jana.
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mwandege ambao ni washindi wa tatu katika mashindano ya Ulega Cup baada ya kupata kichapo jana na timu ya Tengelea katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
Vijana wakionyesha vipaji vyao katika mashindano ya Ulega CUP katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Mkuranga.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...