Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia
Waumini wa Kanisa Katoliki la Watakatifu
Wote Jimbo la Mtwara mara baada ya mahubiri.
Kaimu
Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi Askofu Msaidizi wa
Kanisa Katoliki la Watakatifu Wote Jimbo la Mtwara Fr. Patrick Mwaya mifuko 200
ya Saruji ili kutimiza Ahadi ya Rais aliyoitoa kanisani hapo.
Kaimu
Katibu wa Rais Ikulu, Ngusa Samike(Kushoto) akimkabidhi fedha kiasi cha
Shilingi Milioni 35 kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ili kutekeleza
ahadi aliyoitoa Rais wakati alipopita katika Kijiji cha Somanga na Mnonela.
Katika kijiji cha Somanga Rais Dkt. Magufuli aliahidi kuchangia kiasi cha
Shilingi Milioni 20, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya na kwa upande wa
Mnonela aliahidi kiasi cha Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa
Kituo cha Afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi akisaini kuthibitisha kupokea kiasi hicho cha
fedha ambazo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Magufuli wakati alipofanya
ziara mkoani humo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
katika kituo cha Afya mnonela katika Jimbo la Mtama ambapo aliahidi kuchangia
kiasi cha fedha Shilingi Milioni 15 ambazo tayari Mkuu wa Mkoa wa Lindi
ameshakabidhiwa.
PICHA NA IKULU
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...