Na Bashir
Yakub
1.MGAWANYO WA
WOSIA.
Wosia
umegawanyika mara mbili .
Upo wosia wa
maandishi na upo
wosia wa mdomo.
Wosia hizi zote
zinakubalika alimradi zimekidhi
vigezo vya kisheria
vinavyohitajika.
( a ) Wosia wa
maandishi . Ni wosia ambao
unakuwa umeandikwa.
Unaandikwa na mtoa
wosia na unashudiwa
na mashahidi. Ni wosia
ambao unahimizwa sana
kwakuwa ni wa kuaminika zaidi.
( b ) Wosia wa mdomo. Huu
ni wosia ambao
haukuandikwa isipokuwa aliyeutoa
alitamka tu kwa
maneno. Ni wosia unaokubalika
ikiwa utakidhi vigezo vya kisheria.
2. MASHAHIDI
WANAOTAKIWA KUSHUHUDIA WOSIA.
( a ) WOSIA WA
KIKIRISTO.
Sheria
inayotumika kwa wosia
unaoandikwa na mtu
aliyeishi maisha haya
inajulikana kama “The
Indian Succession Act
1865”. Kwa wakristo
wanaoandika wosia ni
sharti kufuata misingi
ya sheria hii ili
wosia zao kuwa
halali.
Sheria hii imezigawa
wosia mara mbili.
Kwanza wosia wa
upendeleo( privileged will) ulio
katika kifungu cha 52
cha sheria hiyo na
wosia usio wa
upendeleo( unprivileged will)
ulio kifungu cha 50.
Wosia wa
upendeleo ni wosia
unaoruhusiwa kutolewa na
watu maalum kwa mfano
wanajeshi wanapokuwa vitani
na mabaharia wanapokuwa
baharini huko bahari
ya mbali .
Wosia usio wa upendeleo
unawahusu watu wa
kawaida wasio hao waliotajwa. Unaitwa wa
upendeleo kwasababu
wamepunguziwa masharti kutokana
na mazingira wanayokuwemo.
Kwa mujibu wa
kifungu cha 52
wosia wa upendeleo ukiwa wa maandishi
sio lazima kuwa
na mashahidi au
kuwa na sahihi
ya mtoa wosia. Maandishi tu
yasiyo na mashahidi
yanakubalika na ndio
maana unaitwa wa
upendeleo. Na kama ukiwa wa
mdomo basi mashahidi
wawili wanahitajika ili
ukubalike.
Kwa wosia Usio
wa upendeleo unaotumiwa na
watu wa kawaida
mashahidi wanaohitajika ni watu
wawili au zaidi
kwa mujibu wa
kifungu cha 50. Mtu
mmoja hakubaliki kuwa
shahidi. Mashahidi hawa
hutakiwa kumshuhudia mtoa
wosia akisaini wosia.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...