Na Bashir Yakub
1.KUNYIMWA MTOTO.
Wako watu ni
wazazi na wamezaa
lakini wameyimwa watoto.
Zipo sababu nyingi
zinazopelekea hili. Matukio ya
namna hii hayawatokei
sana wanawake na badala yake
wanaume ndio waathirika
zaidi katika hili . Ni rahisi
na kawaida mno mwanaume
kuambiwa na mzazi
mwenzake kuwa huyu
mtoto si wako
hata kama anajua kabisa huyo
mwanaume ndiye mzazi
halisi . Leo haya sio
maajabu tena.
Upo usemi wao
kuwa mwanamke ndiye
anayejua baba wa
mtoto. Sitaki kueleza ukweli
au upotoshi wa
usemi huu bali nawaza iwapo
ni sawa kutumia usemi
huu kupora haki
ya uzazi wa mtu
ambaye unajua kabisa
ndiye mzazi halisi.
Na kwa bahati mbaya
wanaokutwa na kadhia
hii wamekuwa hawajui ni
hatua zipi wachukue. Wapo wanaoamua kufanya vurugu, wapo
wanaojiua, wapo wanaoamua kumuachia
mola, na wengine hukimbilia
serikali za mitaa
ikiwa ni pamoja
na hatua nyinginezo
zisizofaa.
Ukweli ni kuwa
hatua hizo haziwezi
kukusaidia zaidi utapoteza
muda mwingi, gharama
na pengine kuzua
matatizo mengine ambayo
hayakuwako.
Basi sasa
yafaa ujue kuwa
sheria imetambua jambo
hili na imeweka
taratibu nzuri za
kufuata ili kuondoa
ujeuri wa aina
hii.
Sheria Namba 21, Sheria
ya Mtoto ya
mwaka 2009 imeeleza
nini ufanye kama
tutakavyoona hapa chini.
Lakini kabla ya
hilo hebu kwa
kutaja tu tuone sababu
kadhaa zinazofanya wazazi
hasa wa kike kuwanyima wazazi
wenzao haki ya kutambulika kama
wazazi wenzao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...