Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amelaani na kukemea vikali vitendo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji
vinavyoendelea katika jamii na amewataka wananchi kote nchini
kushirikiana katika kukabiliana na vitendo hivyo nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo tarehe 8-March-2017 wakati akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji wa Tanzania (TBC) mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema vitendo hivyo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinamchukiza sana hivyo ametoa wito maalum kwa wananchi na wadau wote bila kujadili dini, kabila wala rangi kupambana ipasavyo na vitendo hivyo ambavyo vinarudisha nyuma jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.
Kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anafurahishwa na hatua na jitihada zinazochukuliwa na wanawake kote nchini katika kujikwamua kiuchumi kwa kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali katika kuelekea katika uchumi wa viwanda.
Amesema jukumu kubwa la serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanawake wanaboreshewa ipasavyo mazingira ya kufanyia kazi hasa shughuli za ujasiriamali ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
“Inapofika katika shida zetu wanawake ni lazima tuwe na kitu Kimoja na sauti Moja katika kulinda na kutetea haki zetu bila kujali itikadi za kisiasa”Amesisitiza Makamu wa Rais.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...