Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na
Mbunge wa Kyela , ameshudia zoezi la kuingizwa majini kwa Meli mpya ya
pili ya mizigo iitwayo MV Ruvuma kwenye bandari ya Itungi, Wilayani
Kyela.
Tukio hilo la kuiingiza Meli hiyo making
limefanyika Machi Mosi . Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya
tani 1000 inaungana na Meli nyingine mpya MV Njombe yenye uwezo wa
kubeba zaidi ya tani 1000 ambayo iliingizwa majini siku tano zilizopita.
Meli zote mbili zipo kwenye hatua ya mwisho ya utengenezaji na
majaribio kabla hazijaanza rasmi kubeba mizigo kwenye ziwa Nyasa.
Tayari
wateja mbalimbali wamejitokeza kutaka mizigo yao ianze kubebwa yakiwemo
makampuni yanayojishughulisha na biashara ya makaa ya mawe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...