NA EVELYN MKOKOI -RUFIJI
NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira, Luhaga Mpina amebaini madudu katika matumizi ya sh. milioni 396 za ufadhili wa Mfuko wa nchi maskini zaidi duniani (LDCF) chini ya mkataba wa dunia mabadiliko ya tabianchi katika utekelezaji wa mradi wa upandaji na uendelezaji wa mikokokatika delta ya kaskazi mto Rufiji.
Katika mradi huo matumizi ya zaidi ya sh.
milioni 364 mchanganuo wake
hauridhishi huku vikundi vinavyodaiwa kulipwa fedha hizo vikikana kulipwa na kusema hawakuwa na mkataba bali walifanya kazi kama vibarua kwa posho ya sh. 10000 kila wanapomaliza kazi na hawakuwa na mkataba.
Kutokana na hatua hiyo Mpina amemuagiza Mkaguzi
wa ndani Ofisi ya Makamu wa Rais, Mwatano Maganga kuhakikisha ndani ya mwezi
mmoja anafanya uhakiki wa matumizi ya fedha hizo za mradi na kuelekeza hatua za
kuchukua kwakuwa
vielelezo alivyokabidhiwa na Msimamizi wa mradi kutoka Halmashauri ya
Rufiji Sabastian Gaganijas vina mashaka. “Naagiza ukaguzi ufanyike, lazima kuna
ubadhilifu umefanyika katika utekelezaji wa mradi, baada ya ukaguzi makini,
tutajua ukweli na kubaini hatua gani zitachukuliwa.” Alisisitiza Mpina.
Hata hivyo, baada ya zoezi zima la kukagua
Delta hiyo yenye kilomota zaidi ya 5 Naibu Waziri Mpina, alisema amesikitishwa na jutekelezaji wa mradi huo unaotumia fedha za wafadhili zaidi ya sh.milioni 396
kuwa na madudu na amejionea mwenyewe kuwa,
mradi hauna usimamizi na kusema kuwa, kuna dalili ya fedha hizo kutumika ndivyo sivyo kwakuwa hata hekta 792 kati ya
1000 zilizodaiwa zimepandwa ni udanganyifu wa wazi.
“Huu ni uhuni ambao haukubali kwa serikali
hii awamu ya tano tuliposema
hapa kazi tu tulimaanisha kuwa hatuwezi kudanganywa watu wamezoea kuona Waziri hawezi kuja kwenye mazingira kama haya nimejionea mwenyewe mikoko iliyopandwa haendani na thamani ya matumizi ya fedha hizo na sehemu kubwa imevamiwa na kupandwa mpunga badala ya mikoko,”alisema.
Alisema katika mchanganuo aliokabidhi na
msimamizo wa mradi fedha hizo
zaidi ya sh.milioni 364 zimedaiwa matumizi yake ni pamoja na kulipa
vikundi 28 vilivyokabidhiwa mradi ambavyo sasa havipo.
Alisema cha kushangaza katika fedha hizo kipo
kikundi kimelipwa zaidi ya
milioni 30 kwa kupanda hekta 3 huku kingine kikilipwa milioni 3 kwa hekta
hizo hizo.
Baadhi ya wakazi wa rufiji wakizungumza
katika ziara ya Naibu Waziri Mpina, wametoa changamoto zao katika kukabiliana
na uharibifu huo wa Mazingira na kuiomba Serikali kuongeza usimamizi
madhubuti katika mradi huo ili kukubaliana na uharibifu huo wa hifadhi hiyo ya
mikoko,
Awali Imeelezwa na mtaalam wa Mazingira
kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw.
Cretus Shengena kuwa, uharibifu huo waMikoko unaweza kusababisha kupotea kwa
uoto asili na baiyonuwai katika eneo hilo kama udhibiti wa dhati usipo
chukuliwa kwa haraka kuinusuru eneo hilo la Delta ya Rufiji kaskazini.
Mradi huo wa hifadhi ya taifa ya Delta ya
Rufiji kaskazini unafadhiliwa na Mfuko wa kundi la nchi maskini zaidi duniani
(LDCF) kupitia Shirika la umoja wa Mataifa ya Mazingira chini ya usimamizi wa
Ofisi ya Makamu wa Rais.
Naibu Waziri
Mpina (katikati) akiwa na ujumbe wake, akisisita jambo wakati wa ukaguzi wa
mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika Delta ya Rufiji kaskazini.
Naibu Waziri
Mpina (kaikati) na Ujumbe wake katika
picha wakitembea kukagua mikoko iliyopandwa katika Delta ya Kaskazini Rufiji.
Naibu Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake
wakiwa katika boti wakielekea katika ukaguzi wa upandaji na utunzaji wa
Mikoko, pamoja na uharibifu wa Mazingira katika Delta ya Rufiji Kaskazini.
Naibu Waziri
Mpina akiwaasa wasimamizi wa mradi wa upandaji na utunzaji mikoko katika delta
ya kaskazini Rufiji hawapo pichani wamueleze ukweli kuhusu matumizi ya fedha na
hali halisiya mradi kabla ya kwenda kukagua upandaji, utunzaji wa mikoko na
uharibifu wa mazingira.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...