Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewataka wasimamizi wa miradi ya matengenezo ya barabara kuzingatia taaluma na weledi husika ili kupata thamani ya fedha kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu husika bila kukiuka taratibu za manunuzi.
RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua kikao cha bodi ya barabara ya mkoa wa Dar es Salaam kilichofanyika katika ukumbi wa Arnautoglo na kuwaomba mameya, madiwani, wakuu wa wilaya na wakurugenzi kuifuatilia miradi hii kwa karibu, huku akishauri kuwa ni vyema miradi hii ikafanyika kwa gharama nafuu, kwa muda mfupi na kwa viwango, kwani fedha za wananchi ndiyo zinatumika wanapaswa kutendewa haki kwa kuona matokeo chanya kwenye miradi ya maendeleo.
Katika hatua nyingine kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited kupitia Mkurugenzi wake Maida Waziri ameeleza kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, haina vumbi wala uterezi na ujenzi wake hutumia muda mfupi na kuishauri serikali kutumia ujenzi huo wa gharama nafuu kwa takribani asilimia 50, huku akizitolea mfano Australia na Algeria kuanza kutumia ujenzi huo, hivyo hiyo ni suluhu ya lawama za muda mrefu kuhusu barabara mbovu nchini.
Bwana Fabian Campagnolo kutoka kampuni ya ujenzi ya IBRA Contractors Limited , akitoa maelezo kwa wajumbe wa kikao hicho cha barabara , kuhusu ujenzi wa barabara zinazotumia teknolojia ya kisasa kwa udongo wa kawaida ni bora na huweza kudumu zaidi ya miaka 10, katika ukumbi wa Arnautoglo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...