Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini (Tanesco).Mradi huo umezinduliwa rasmi kitaifa katika kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga.
Na Zuena Msuya, Tanga
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amezindua rasmi
mradi wa usambazaji wa umeme vijijiji ,unaotekelezwa na Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu kitaifa kwa kushirikiana na Shirika la
Umeme nchini Tanesco,utakao sambaza umeme kwa vijiji vyote ambavyo
havikupata huduma hiyo wakati wa REA Awamu ya Kwanza na ya Pili.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Zingibari
wilayani Mkinga mkoani Tanga, Dkt . Kalemani alisema kuwa, REA Awamu
ya Tatu itatekelzwa kwa miaka mitano kuanzia sasa hadi kufikia 2021.
Dkt. Kalemani alifafanua kuwa,mara baada ya uzinduzi rasmi wa kitaifa wa
mradi huo mkoani Tanga,Mikoa mingine itaendelea kuzindua mradi huo
katika mikoa yao kulingana na makubaliano ya mikataba ya wakandarasi
husika katika Mikoa hiyo.
"REA awamu ya Tatu imezinduliwa rasmi hapa mkoani Tanga, mradi huu
sasa utamaliza kazi ya kuunganisha huduma ya umeme katika vijijini vyote
7867 nchini vilivyoachwa katika Awamu ya Kwanza na ya Pili ya mradi huo,
ili kifikia idadi ya vijiji vyote 12,262,Tanzania bara ifikapo mwaka 2021",
alisema Kalemani.
Akizungumzia mradi huo kwa Mkoa wa Tanga, Dkt. Kalemani alisema
kuwa REA Awamu ya Tatu itasambaza huduma ya umeme katika vijiji 166,
ambapo vijiji 20 kati ya hivyo ni vile ambavyo vilipitiwa na Mradi wa REA
Awamu ya Kwanza na ya Pili lakini havikuunganishwa na huduma ya
umeme , na vijiji 146 ambavyo havikupitiwa kabisa wala kuunganishwa na
Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini iliyopita.
Aidha , Dkt. Kalemani alitoa wito kwa wakandarasi watakaotekeleza Mradi
wa REA Awamu ya Tatu, kutekeleza majukumu yao kwa wakati kwa
kuzingatia uhitaji wa huduma ya umeme nchini ili kutimiza azma ya Serikali
ya kuwa nchi ya viwanda.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela aliwataka
wakazi wa Mkoa huo waliokosa huduma hiyo katika miradi iliyotangulia,
kutandaza nyaya za umeme katika nyumba zao ili kuweza kuunganishwa
na huduma ya umeme ambayo hupatikana kwa bei nafuu ya shilingi elfu
27 .
Aidha aliwataka wananchi hao kulinda na kuitunza miundombinu ya mradi
huo kwa maslahi ya taifa na wananchi kwa ujumla kwa kuwa miundombinu
hiyo ni ya gharama kubwa.
Wakazi wa kijiji cha Zingibari Wilayani Mkinga mkoani Tanga wakisikiliza
hotuba ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (
hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa usambazaji wa umeme
vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu,
kwa kushirikiana na Tanesco.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani,(katikati), Mkuu
wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela( kushoto) na Naibu Waziri, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhaga Mpina(kulia) wakiwa
katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga, Mawaziri hao walikuwa mkoani humo
kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, akisalimiana na
wakazi wa kijiji cha Zingibari wilayani Mkinga mkoani Tanga alipofika kijijini
hapo kuzindua rasmi mradi wa usambazaji wa umeme vijijini kitaifa
unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Tatu, kwa
kushirikiana na Tanesco.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...