Na Benny Mwaipaja, WFM

Naibu Waziri Wizara ya Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali inaendelea kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika kuhakikisha miradi yote ikiwemo ile inayofadhiliwa na Benki hiyo inatekelezeka kwa ufanisi Mkubwa.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na Wakurugenzi Watendaji 12 wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika Mkutano uliofanyika Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dar es salaam, baada ya ujumbe huo kutembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Benki hiyo hapa nchini.

“Madhumuni makubwa ya ziara ya Wakurugenzi watendaji wa Benki ya AfDB waliokuja nchini tangu Februari 25, ni kukaa pamoja na Serikali ili kujadiliana kuhusu sera na mipango mikakati ya maendeleo, lakini pia kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa kupitia ufadhili wa Benki ya hiyo” Alifafanua Dkt. Kijaji.

Wakurugenzi hao ambao ndio watoa maamuzi katika Benki hiyo, wametembelea miradi ya maji Zanzibar na kwa upande wa Tanzania Bara wametembelea mradi wa kufua umeme wa Sokoine substation uliopo Manispaa ya Ilala.

Katika Mkutano huo, Serikali ya Tanzania imeendelea kuiomba Benki ya AfDB kuharakisha kazi za upembuzi yakinifu na hatimaye kutoa fedha ili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo uanze mapema kwa kadri inavyowezekana.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji (Mb) akisisitiza kuhusu jitihada zinazofanywa na Serikali katika kutatua changamoto ya deni la Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kwa kuendeleza juhudi za kutumia nishati mbadala ya Gesi badala ya Mafuta mazito katika kuendesha mitambo ya Uzalishaji wa umeme, katika kikao na Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)(kushoto) akiongoza Mkutano wa Wakurugenzi Watendaji wanaoziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), katika kufanya tathmini ya maendeleo ya Miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo, ambapo Wakurugenzi hao waliipongeza Tanzania kwa kutekeleza miradi kwa ufanisi. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi Lekhethe aliyeongoza ujumbe wa Wakurugenzi Watendaji wengine 12 (hawapo pichani), katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi Lekhethe (kulia) wakipeana mikono baada ya kumalizika kwa mkutano wa tathmini ya maendeleo ya Miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo nchini Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wanne kulia) na Mkurugenzi Mtendaji kutoka Afrika ya Kusini Bi. Mmakgoshi Lekhethe (wa tano kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi Watendaji wanao ziwakilisha nchi zao katika Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), baada ya kumalizika kwa mkutano wa tathmini ya maendeleo ya Miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo nchini Tanzania, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...