Wataalam wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini kuanzia leo tarehe 05 Machi, 2017 wako katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya umeme pamoja na kukutana na wadau wa nishati jadidifu.
Mkurugenzi
Mtendaji kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro
Electric Company, Alex Andoya (katikati) akielezea maendeleo ya kampuni hiyo katika uzalishaji wa umeme mara
baada ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini kufanya
ziara katika kampuni hiyo, Mbinga mkoani Ruvuma ili kujionea maendeleo ya
shughuli zake. Wataalam hao wako katika ziara ya kukagua miradi ya umeme pamoja na kutoa
ushauri wa kitaalam.
Mtaalam
kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric
Company, Mhandisi Jasper Bubelwa (kulia)
akielezea mfumo wa uendeshaji mitambo wa
kampuni hiyo
Wataalam
wa Nishati Jadidifu, Emillian Nyanda,
(wa pili kutoka kulia) na Mhandisi Stephan Kashushura ( wa pili kutoka kushoto)
wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Kampuni ya Kuzalisha Umeme
kwa Kutumia Maji ya Andoya Hydro Electric Company mara baada ya kumaliza ziara
katika kampuni hiyo. Kushoto kabisa ni Fred Tawete kutoka Wizara ya Nishati na Madini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...