Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nauye ameahidi kuilinda tasnia ya Habari, wanahabari na wanaowekeza katika tasnia hiyo ili uwekezaji usiharibiwe ovyo.

Nape amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiongea na wafanyakazi wa kituo cha redio cha EFM mara baada ya kumaliza ziara yake  ofisini hapo na kushuhudia uwekezaji mkubwa uliofanywa na mkurugenzi wa Kituo Hicho. Amesema, Serikali itaipa EFM ushirikiano na msaada watakaohitaji ili kuhakikisha uwekezaji uliowekwa unasonga mbele.

Ameongeza kuwa, kituo hicho kimefanya uwekezaji mkubwa na kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania  wengi hasa kwenye taaluma ya Habari. " Msikatishwe tamaa na kelele za Barabarani, kazi mnayofanya mafanikio yenu ni makubwa, kazi yenu ni kubwa".

Aidha waziri Nape amekipongeza kituo hicho kwa kupewa kibali cha  kurusha matangazo yake ya redio katika mikoa kumi.

Aliongeza kuwa anaimani kuchaguliwa kwa EFM kwenda mikoa hiyo kumi kutaifanya tasnia ya Habari kuwa juu hasa katika sekta ya Michezo ambayo kituo hicho kimeonyesha njia ndefu ya kukimudu.

 Amewaasa kwenda kufanyia kazi kibali hicho kwa umakini zaidi na kuwaomba TCRA, kutokutoa adhabu Mara kwa Mara bali watumie njia ya kukanya zaidi.

Naye Meneja mkuu wa Kituo hicho Denis Sebo amesema TCRA wamewapa kibali cha kurusha matangazo yao ya redio katika mikoa kumi ikiwemo Dar es Salaam.

Amesema wamepokea kwa Furaha kibali hicho na kwamba wameishaanza maandalizi na mwezi huu watarusha matangazo katika moja ya mikoa mipya.

Aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Mbeya, Tanga, Mtwara, Babati, Mwanza  Moshi,Tabora , Sindida na Kigoma
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (wa pili kushoto) akiwa pamoja na uongozi wa kituo cha redio 93.7 Efm wakati alipotembelea kituo hicho asubuhi hii ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoianza ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. kushoto kwake ni Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM, Francis Ciza (Dj Majay) na kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Redio EFM, Dennis Ssebo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza jambo wakati akifanyiwa mahojiano katika moja ya vipindi vya redio hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...