Hapa Kazi Tu!! Ndivyo Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Bi. Rehema Madusa anafanya mara baada ya yeye pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya yake kuungana kwa pamoja na kuamua kuanza kuitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo miradi ya miundombinu kama barabara na majengo mengine ya kiserikali na ya kijamii kama Ujenzi wa Zahanati, Kituo cha Afya na Ujenzi wa maabara kwa shule za Sekondari. 

Katika Ziara hiyo aliyoianza hivi karibuni,DC Madusa alibaini changamoto mbalimbali na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ili kuwezesha gurudumu la maendeleo kusonga mbele. 

Aidha, DC Madusa akizungumza na mtandao huu amesema amejipanga kikamilifu kuhakikisha Shule za Sekondari za Wilaya hiyo zinakua za mfano kwenye mitihani kwa ngazi ya Mkoa, Kanda na Taifa kwa Ujumla, hivyo amewataka wananchi wake kumuunga mkono ikiwemo kuhakikisha nidhamu ya wanafunzi inatazamwa kwa jicho la karibu ili kuwasaidia walimu kufanya majukumu yao pasi na matatizo yeyote
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mhe. Rehema Madusa akitoa maelekezo  kwa mfadhili kuondoa bati zisizotakiwa (G. 30) na kupaua kwa bati zenye viwango vilivyopitishwa na serikali (G. 28) katika moja ya shule huko mjini Chunya mkoani Mbeya.Na Mr.Pengo wa Globu ya Jamii Mbeya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...