D: MTU WA MISIMAMO
Baada
ya kumaliza darasa la nane Tabora, alipata nafasi ya kusoma chuo kikuu
cha Makerere Uganda. Alisomea ualimu na alihitimu diploma mwaka 1947.
Aliporudi Tanganyika, alipata nafasi ya kazi kutoka misheni na
serikalini. Serikalini kulikuwa na mshahara mkubwa na marupurupu mengi
kuliko misheni lakini alikataa kufanya kazi serikalini akipinga mfumo wa
tofauti kubwa ya malipo.
Misimamo
yake ya kupinga sera za kikoloni ilimgharimu kwani serikali ya kikoloni
ilikataa kumpa nafasi ya masomo nje ya nchi. Ni kwa utetezi tu wa
rafiki yake mkubwa, Father Walsh, ndipo alipokubaliwa kwenda kusoma chuo
kikuu cha Edinburgh cha Scotland Uingereza, aliposomea historia, uchumi
na falsafa.
E: MTU WA KUJISHUSHA
Chuoni
Edinburgh alihitimu na kupata Masters na kuwa mtanganyika mweusi wa
kwanza kupata mafanikio hayo. Hata hivyo, hakupata kiburi na aliporudi,
akaenda kijijini kwao Butiama ambapo alijenga kwa mikono yake mwenyewe
nyumba yake ili afungie ndoa na mchumba wake Maria Magige. Alichanganya
saruji na mchanga yeye mwenyewe na kufyatua matofali. Wanakijiji
walimshangaa msomi kama yeye kushika tope...wasomi wa wakati huo, wengi
wao darasa la nne tu lakiji walikuwa daraja la juu sana.
F: MSHAWISHI
Alijiunga
na harakati za siasa chini ya TAA. TAA hakikuwa chama cha siasa moja
kwa moja bali kikundi cha kudai baadhi ya haki ambazo zilikuwa za
wazungu pekee. Akawashawishi wazee aliowakuta wabadili malengo na
kuanzisha chama rasmi cha siasa kitakachodai uhuru kamili badala ya haki
fulani pekee. Wazee wakakubali na kuanzisha TANU, Julai 7, 1954 na yeye
akawa mwenyekiti. TANU ikafanikiwa kuleta uhuru, 1961.
Lakini
ushawishi mkubwa kabisa katika historia yake na ya nchi ni ule wa mwaka
1958 aliposhawishi wajumbe wa TANU kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa
baraza la kutunga (LEGCO). Vyama mbalimbali vilitakiwa kushiriki na
chama kitakachopata wajumbe(wabunge) wengi ndicho kitakachounda
serikali.
Huu
ndiyo uchaguzi wa kwanza kabisa nchini na mkoloni aliweka masharti
magumu kwa waafrika kupiga ili kukandamiza haki zao. Masharti hayo ni
kuwepo kwa viti vitatu vitakavyoshindaniwa kwa matabaka(wazungu, waasia
na waafrika) huku waafrika wakitakiwa kupiga kura zote tatu. Lengo la
mkoloni lilikuwa kuhakikisha baraza la kutunga sheria linakuwa na
wajumbe sawa, yaani waafrika, wazungu na wahindi. Kutokana na sharti
hili, uchaguzi huu uliitwa UCHAGUZI WA KURA TATU.
Masharti
mengine ya kumuwezesha mwafrika kupiga kura ni kuwa na kipato cha pauni
mia nne za Uingereza kwa mwaka, pia awe na kiwango cha elimu ya darasa
la 12(form four) na awe ameajiriwa katika kazi maalumu.
Masharti haya yaliwakera wazee na wanachama wa TANU. Viongozi wa makao makuu na majimboni wakapanga kuususia.
Nyerere
peke yake alitaka TANU ishiriki uchaguzi huu kwa sababu alihisi kama
ingesusa, chama cha wazungu cha United Tanganyika Party(UTP) kingepata
mteremko na kuzoa viti vyote na kuingia kwenye baraza la kutunga sheria
huku TANU kikibaki nje. Kupitia fursa hiyo, wazungu wangetunga sheria
kali zaidi za kuchelewesha uhuru kwa kisingizio kwamba waafrika hawajawa
tayari kujitawala huku mfano ukiwa kususia uchaguzi.
Nyerere aliona mbali zaidi ya wenzake ndani ya chama.
Nyerere aliona mbali zaidi ya wenzake ndani ya chama.
Uchaguzi
huo ulipangwa kufanyika Septemba 1958, TANU ikapanga kufanya mkutano
wake mkuu wa mwaka wa 1958 mjini Tabora kuanzia Januari 21-26, 1958
kuamua hatima ya uchaguzi.
cc. Zaka Zakazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...