Shirika
la Anga la Etihad limetangaza uteuzi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Idara
yake tanzu ya Airline Equity partners, Bwana Robin Kamark ambaye
atashughulikia kuongoza na kuendeleza mikakati ya uwekezaji
inayojumuisha wabia wa Shirika hilo kama vile; Airberlin, Alitalia, Jet
Airways, Air Serbia, Air Seychelles, Etihad Regional na Virgin
Australia.
Mtendaji huyo mkuu atakuwa chini ya Rais wa Shirika
hilo na Mkurugenzi Mkuu. Kamark anachukua nafasi ya Bruno Matheu ambaye
alishika wadhifa huo tangu Mei 2016 ambaye imeelezwa kwamba anaachia
ngazi kutokana na sababu zake binafsi.
Kamark amefanya kazi katika sekta ya anga kwa takriban miaka 17, huku akifanikiwa kufikia malengo ya mikakati yake ya kibiashara na masuala ya utawala katika Shirika la SAS ambako pia alikuwa akitekeleza majukumu yake kama Ofisa Mkuu wa Biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...