Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa katika kuitangaza Serikali. ameyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.
“Napenda nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii kwa mara ya kwanza katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na” Alisema Waziri Mwakyembe.
Amesema kuwa kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo imeonyesha weledi wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara hiyo kuiga mfano mzuri na kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina vipaji na ubunifu wa hali ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya Serengeti Boys na n.k
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema kuanzishwa kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali katika kutangaza matamko mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii husika.
“Sisi kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi zake”,Aliongeza Dkt Abbas.
Mbali na hayo amesema kuwa kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni hii itakuwa mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano waliyofanya na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan Suluhu.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza kitufe kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya
Idara ya Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.Televisheni iyo itaonyesha kazi
mbalimbali za Wizara,Taasisi na Idara za Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu
Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan
Abbas wakifurahi mara baada ya kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya
Habari-MAELEZO jana mjini Dodoma.
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia mahojiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa
Idara ya Maelezo Hassan Abbas na Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu
maadhimisho ya Muungano yatakayofanyika mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya
kwanza kupitia televisheni ya mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza na
menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo Pichani) na
kuipongeza Idara ya habari kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni Naibu Waziri wake
Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na Mkurugenzi Mkuu
Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas. Picha na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...