Katika kutekeleza Mradi wa ujenzi wa Viwanda vya sukari Mifuko ya Hifadhi ya jamii NSSF na PPF ilianzisha kampuni tanzu iitwayo Mkulazi ili kuendesha mradi mkubwa wa viwanda viwili vya sukari katika maeneo ya Mkulazi na Mbigiri Mkoani Morogoro.

Mwishoni mwa wiki Bodi ya Wakurugenzi ya Mkulazi ilitembelea moja ya mradi katika eneo la Mbigiri Mkoani Morogoro ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Mkulazi ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Gadius Kahyarara amesema wametembelea maeneo ambayo ujenzi unaendelea ikiwemo ujenzi wa barabara unaoendelea, ujenzi wa madaraja, na utayarishwaji wa shamba la miwa itakayotumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari katika kiwanda hicho.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa PPF William Erio amesema wameshuhudia kazi kubwa inayoendelea ya maandalizi ya shamba na kuridhishwa nayo. Mkurugenzi Mkuu wa PPF amebainisha kwamba wanatarajia kuanza upandaji wa miwa siku chache zijazo.

Katika ujenzi unaoendelea baadhi ya vijana wasomi wasio na ajira wameanza kujitokeza katika ujenzi wa kiwanda cha sukari Mkoani Morogoro ili kuunga mkono jitihada za Rais wa awamu ya tano ya Ujenzi wa viwanda.

Bodi ya Wakurugenzi wa kampuni tanzu ya Mkulazi inayoundwa na Mifuko ya PPF na NSSF wameridhishwa na jitihda zinazoendelea za ujenzi wa kiwanda baada ya kutembelea na kukagua shughuli zinazoendelea.
Meneja wa shamba la miwa la Mbigiri Prosper Kombe akitoa maelezo kwa Viongozi wa PPF na NSSF kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Mku wa NSSF Profesa Gadius Kahyarara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mkulazi Holding Company, Mkurugenzi Mkuu wa PPF William Erio pamoja na baadhi ya viongozi wa NSSF.
Mjumbe wa Bodi ya Mkulazi Holding Company Martin Mmari ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF akifyatua tofali kwa ajili ya ukarabati wa kiwanda cha sukari Mbigiri.
Meneja Manunuzi wa NSSF Kirondera Nyabuyenze akifyatuaji tofali kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha sukari Mbigiri.
Shughuli za kilimo zikiendelea katika shamba la miwa la Mbigiri Morogoro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...