Mkurgenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari (Kati Kati) Akionyesha Cheti cha Trainair Plus Kilichotunukiwa kwa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Kinachomilikiwa na TCAA. CATC Imefuzu kuwa Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Watumishi wa Chuo Cha Usafiri wa Anga Tanzania(CATC) wakifurahia kutunukiwa Cheti cha Trainair Plus. CATC imetunukiwa Cheti hicho baada ya kufuzu kuwa Mwanachama shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Mkurgenzi Mkuu,Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA), Hamza S. Johari (Kati Kati) Akifungua Cheti cha Trainair Plus Kilichotunukiwa kwa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Kinachomilikiwa na TCAA. CATC Imefuzu kuwa Mwanachama Shirikishi wa Shirikisho wa Umoja wa Vyuo Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Kwa mara nyingine Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania( CATC) kinachomilikiwa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) kimefuzu na kutunukiwa cheti cha kuwa mwanachama Shirikishi wa wa Umoja wa Vyuo Vya Mafunzo ya Usafiri wa Anga Vinavyotambulika na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO).
Cheti hicho ambacho maarufu kama TrainAir Plus, kimetolewa na Shirikisho la TrainAir Plus, wiki hii baada ya CATC kufuzu vigezo na masharti ikiwa ni pamoja na kuandaa mitaala inayokubalika na shirikisho. Kwa mara ya kwanza CATC ilitunukiwa cheti hicho mwaka 2012 na muda wake uliisha mwaka 2015.
Akizungumza katika hafla fupi ya kupokea cheti hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, Hamza S. Johari amewachagiza watumishi wa chuo cha CATC kufanya kazi kwa bidiii na kuhakikisha CATC inaendelea kujiimarisha na kutoa mafunzo bora zaidi.
Hiki ni chuo cha kimataifa kwa kuwa kinatoa mafunzo kwa wanafunzi wa kutoka nje ya nchi, lengo letu tuhakikishe tunakuwa wanachama kamili wa TrainAir Plus, Amesema Hamza . Ameahidi kutoa msaada unaohitajika katika kukiimalisha chuo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha CATC, Aristide Kanje, Amemuhakikishia Mkurugenzi Mkuu kuwa timu yake itaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha chuo hicho kinatakeleza majukumu yake kama inavyotakiwa.
Pamoja na faida nyingine, vyuo wanachama wa TRAINAIR PLUS wana fursa ya chuo kutambulika kimataifa, kupata, kubadilishana mitaala ya masomo ya usafiri wa anga inayoandaliwa kwa kufuata viwango vinavyokubalika kimataifa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...