Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amefanya kikao cha kazi na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Taasisi ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kujadili mafanikio na changamoto katika utendaji kazi wa Wizara.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akizungumza na watendaji pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake (hawapo pichani) katika kikao hicho. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. James Mdoe (kushoto) akielezea mafanikio ya sekta za nishati na madini nchini katika kikao hicho.
Sehemu ya watendaji na wafanyakazi kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) katika kikao hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...