Na Bashir Yakub.
1. WAHUSIKA
Walalamikaji(petitioners) ni wawili. Wa kwanza Raila Amolo Odinga na wa pili Stephen Kalonzo Musyoka, mgombea mwenza.
Walalamikiwa(respondents) ni watatu, wa kwanza ni tume huru ya uchaguzi IEBC. wa pili mwenyekiti wa tume hiyo ndg Wafula Chebukati na watatu ni ndg Uhuru Muigai Kenyatta.
Pia kuna walioomba kuingia katika kesi hiyo na kukubaliwa. Wa kwanza mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ameingia kama rafiki wa mahakama(amicus curiae) , wa pili chama cha wanasheria kenya "Law Society of Kenya LSK," nao kama rafiki wa mahakama.
Wa tatu na nne ni Dr Ekuru Aukot na Mr. Michael Wainaina ambao wameingia kama wahusika wenye maslahi(interested parties). Hawa nao walikuwa wagombea urais.
2. MUDA WA KESI.
Kwa katiba ya Kenya mlalamikaji anazo siku 7 tu za kufungua shauri tokea siku matokeo yalipotangazwa. Na mahakama inazo siku 14 tu za kusikiliza na kutoa hukumu tokea siku shauri lilipofunguliwa.
Kesi hii imekuwa ikisikilizwa mpaka usiku saa tano zikiwemo siku za jumamosi na jumapili ili kuendana na muda wa katiba.
3. MAHAKAMA NA MAJAJI.
Mahakama inayosikiliza ni mahakama ya juu( the supreme court).
Majaji wanaosikiliza ni 7 wakiomgozwa na Jaji mkuu David Maraga na naibu wake mwanamama Philomena Mwilu. Wengine ni Jackton Ojwang, Mohammed Ibrahim, Njoki Ndung'u, Smokin Wanjala na Isaac Lenaola.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...