Arusha: Kampuni ya Kansai Plascon Afrika ltd. Ambayo ni kampuni tanzu ya kampuni ya rangi ya Kansai iliyoko Japan, imehitimisha makubaliano yake ya kununua shughuli za rangi za Sadolin nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.  Hii ilitangazwa na Deodatus Makumpa Meneja wa Kanda ya Kaskazini, Plascon Tanzania wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari katika Hotel ya Arusha Jijini Arusha.

Kampuni ya rangi ya Kansai ni kampuni ya kimataifa ambayo inaendesha shughuli zake nchini Japan, China, Mashariki ya Kati, Ulaya na Afrika. Bidhaa zake inazotoa zinajumuisha upambaji, Viwanda, rangi za kulinda na mitambo, ina vituo vya utafiti na maendeleo nchini Japan, India na Afrika Kusuni.

“Tumefurahishwa na mafanikio haya. Kupitia haya, tutaweza kutumia nembo yenye nguvu ya urithi wa Kansai, uwezo wa kimataifa wa kiufundi, na utendaji wa kuaminika, kutupatia uwezo mpya, kuweza kupata teknolojia mpya na utambuzi ambao ni muhimu zaidi katika kuendelea kukuza nembo hii,” alisema Makumpa
 
Akiongea kuhusu sababu za kuinunua, Gary van der Merwe, Rais wa Kampuni ya Plascon Afrika Mashariki alisema kwamba makubaliano haya yanadhihirisha nia ya Kansai Plascon katika kujiendeleza zaidi duniani. “Afrika Mashariki ni moja kati ya ukanda ambao unakuwa haraka zaidi kiuchumi barani Afrika. Kwa ukuaji wa kasi wa daraja la kati, kuongezeka kwa nguvu ya utumiaji na kukua kwa miji, huu ni muda muafaka wa kuingiza sokoni bidhaa zetu mbali mbali kwaajili ya kuboresha zaidi mtindo wa maisha yao wakati huo huo tukiwa tunaongeza kuenea kwetu duniani”.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...