Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

Hatimaye Raia wa Afrika Kusini, Menelaos Tsampos anayekabiliwa na tuhuma za kutishia kwa njia ya mtandao amepatiwa masharti ya dhamana.

Amesomewa masharti hayo na hakimu mfawidhi Cyprian Mkeha wa mahakama ya Hakimuh Mkazi kisutu ambapo anatakiwa kuwa na wadhamini wawili wataoweka dhamana ya sh.milioni 20.

Hakimu Mkeha amesema, katika wadhamini hao wawili mmojawapo lazima awe ni raia wa Tanzania na ikitokea mdhamini mwingine ni raia wa nje ya nchi lazima awasilishe hati yake ya kusafiria mahakamano, mshtakiwa pia anatakiwa kuwasilisha hati yake ya kusafiria mahalamani na antakiwa kuripoti katika kituo cha polisi cha kawe mara moja kwa wiki.

Kabla ya kusomewa masharti ya dhamana, Hakimu Mkeha amesema
Hakuna sababu ya mshtakiwa kunyimwa dhamana eti kwa sababu ni raia nje na pia katika Maelezo yaloyotolewa inaonyesha hati yake ya kusafiria iko polisi.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa manne ambapo anadaiwa June 22/2017 maeneo ya DSM kupitia mfumo wa Kompyuta alituma ujumbe wa E-mail uliokuwa na maneno ya vitisho kwa mtu anayeitwa Costa Gianna, ikiwa ni kinyume na sheria ya mtandao kifungu cha 23(1) na (2) namba 14 ya mwaka 2014.

Pia anadaiwa kukutwa na visa ya kugushi na kwamba ameishi nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka minne bila kuwa na kibali
Raia wa Kusini, Menelaos Tsampos anayekabiliwa na tuhuma za kutishia kwa njia ya mtandao, kuishi nchini bila kibali na kupatikana na visa ya kughushi akijadiliana na mawakili wake mahakamani hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...