Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza waendesha
bodaboda wote nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa na kofia ngumu ‘Helmet’
ndani ya mwezi mmoja baada ya hapo hatua kali zitachukuliwa.
Mheshimiwa
Nchemba ametoa agizo hilo jana Agosti 26,2017 mjini Shinyanga
wakati akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' zaidi ya
300 wanaofanya shughuli zao katika manispaa ya Shinyanga.
Alisema
kosa la kutovaa kofia ngumu litawahusu wamiliki wa bodaboda,waendesha
bodaboda pamoja na abiria ambao kwa pamoja watawajibika kila mmoja kwa
nafasi yake.
“Hili
litafsiriwe vizuri kila eneo katika nchi yetu,kwanza kabisa kama
mmiliki hajaweka kofia mbili,bodaboda ikikutwa haina kofia mbili,tatizo
lile linaenda kwa mmiliki,pili kama mwendesha bodaboda amepewa kofia
mbili halafu akaamua kuziacha huyo ana kosa”,alieleza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli 'daladala' jana mjini Shinyanga.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule.Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Mkazi wa Shinyanga Mjini akieleza shida yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba baada ya kikao kufungwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...